Ahadi ya meli kwa maziwa matatu inaenda vyema - Dk. Mwakyembe
Mei, 2013
Serikali imesema utekelezaji wa ahadi ya kujenga meli tatu katika ziwa Viktoria, Tanganyika na Nyasa unaenda vizuri na unategemewa kukamilika kabla ya mwaka 2015.
Dk. Mwakyembe amesema Tanzania inawasiliana na Serikali ya Korea Kusini kupitia Benki ya Exim kupata mkopo wenye masharti nafuu kujenga meli tatu za abiria na mizigo katika maziwa hayo.
Amesema kumekuwa na ukuwaji wa shehena na makasha katika mwambao wa Bandari na kuongeza kuwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo umeanza utekelezaji wake baada ya Serikali kusaini mkataba na Serikali ya Watu wa China, Machi 23, mwaka huu.
Kuhusu Bandari ya Mwambani, Dk. Mwakyembe amesema tayari zabuni imetangazwa ili kumpata mwekezaji kwa ajili ya kuendeleza Bandari hiyo kwa mpango wa ubia.
Chanzo: Hotuba ya Waziri wa Uchukuzi, Bungeni Dodoma Mei, 2013
_______________________________________________________________________
Bandari ya Mtwara kuwa kitovu cha uchimbaji Gesi Baharini-Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Wanamtwara watanufaika na Mipango ya Serikali ya kuipanua na kuijenga upya Bandari ya Mtwara ili iweze kuhudumia mahitaji ya utafutaji na uchimbaji gesi baharini.
“Pamoja na hayo Bandari ya Mtwara pia itatumika kupitisha vyombo vinavyotumika katika utafiti, uchimbaji na uendelezaji wa gesi,” ameongeza Dk. Kikwete. Rais ametoa ufafanuzi huo katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa kwanza mwaka 2013, ambapo pamoja na mambo mengine alilenga kutoa ufafanuzi wa harakati za kupinga gesi kusafirishwa kutoka Mtwara.
Chanzo: Hotuba ya Rais/Kwa habari zaidi soma TPA Gazeti katika tovuti hii.
________________________________________________________________________
Number of cars Zambian import via Dar Port rises
February 2013
More than 75,000 motor vehicles were imported by Zambians through the Port of Dar es Salaam in 2012 compared to 25,000 for previous year, The Times of Zambia reported recently.
_______________________________________________________________________
Dar port efficiency impresses EU delegates
November 2012
Delegates from the European Union (EU) have been impressed by the initiative taken by the Tanzania Ports Authority (TPA) in making Dar es Salaam port more effective and competitive. The EU mbassador to Tanzania, Mr Filiberto Sebregondi said that during the official visit of the 23 delegation of EU ambassadors and business representatives at the port.
Ufanisi Bandari ya Dar wapongezwa na EU
Novemba 2012
Umoja wa Ulaya (EU) umepongeza jitihada zilizofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika kufanyia kazi mapendekezo yao waliyoyatoa mwaka jana ya kuboresha Bandari ya Dar es Salaam. Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi kwa niaba ya ujumbe wa mabalozi na wafanyabiashara 23 ambao walitembelea Bandari hiyo hivi karibuni.
________________________________________________________________________
Wadau Bandari ya Mtwara Wakutana.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh. Joseph Simbakalia amefungua na kuongoza kikao cha Wadau wa Bandari ya Mtwara ambacho kililenga kujadili mambo mbalimbali hasa miradi ya uboreshaji wa Bandari ya Mtwara.
Kikao hicho kimefanyika Septemba 05, 2012 katika ukumbi wa Makonde mjini Mtwara, ambapo Mkuu wa Mkoa alifungua rasmi mkutano huo majira ya asubuhi na baadae kuongoza majadiliano kuhusu mada mbalimbali zilizotolewa na Wadau wa Bandari hiyo.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Bandari ya Mtwara, Mpango wa Maendeleo ya EPZA na Taarifa ya Maendeleo ya Utafiti wa Gesi na Mafuta katika Ukanda wa Mtwara. Mradi wa maendeleo wa ‘Mtwara Development Corridor’ pia ulijadiliwa kwa kina wakati wa kikao hicho.
Dk. Mwakyembe Afanya Ziara Bandari ya Mtwara.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amefanya ziara katika Bandari ya Mtwara mnamo Septemba 3 na kukutana na viongozi na wadau mbalimbali.
Katika Ziara hiyo Dk. Mwakyembe aliongozana na wadau mbalimbali wa Bandari ya Mtwara ambao wapo mkoani Mtwara kuudhuria mkutano maalumu unaowakutanisha wadau wa Bandari hiyo pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA). Mkutano huo unalenga kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika Bandari ya Mtwara.
________________________________________________________________________