MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

 

  1. Ndugu Wananchi mnatangaziwa kuwa siku ya Ijumaa tarehe 8/11/2019 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) itasafirisha Mzigo wenye vipimo vikubwa kutoka Bandari ya Dar Es Salaam kuelekea Bandari ya Mtwara, Gari litakalotumika lina namba za usajili: SU 43069/SU 41437.

 

  1. Gari lina vipimo vifuatavyo:
  • Urefu - mita 5. 25
  • Upana - mita 3.75
  • Kimo - mita 18

 

  1. Njia itakayotumika: Mandela Road, Kilwa Road Kupitia Lindi hadi Bandari ya Mtwara.

 

  1. Gari litasafiri muda wa mchana tu (Kuanzia saa 12:30 Asubuhi mpaka saa 12:00 Jioni).

 

TPA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

 

Imetolewa na:

 

Menejimenti

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania-TPA

Makao Makuu